# Maelezo ya jumla Kama lugha yako unayotumia haina haitumii maswali yenye majibu ndani ya swali, unaweza kutumia kame sentensi tu. # Kwanini Shetani ameujaza moyo wako...ardhi? Petro alitumia swali hili kumkemea Anania. "Kwa namna gani umemruhusu Shetani kukushawishi ili kudanganya juu ya kiasi cha mauzo ya ardhi yenu." # kusema uongo kwa Roho Mtakatifu na kuficha sehemu ya mali ya shamba Inaonyesha Anania alikuwa amewaambia mitume kuwa alichotoa kilikuwa kiasi chote cha mauzo ya shamba lake # Wakati lilipokuwa halijauzwa, halikuwa ni mali yako? Petro alitumia maswali haya kumkumbusha Anania kwamba alikuwa na uwezo juu ya pesa yake. "Alikuwa na wajibu wa kusimamia pesa yake kwa uadilifu." # Ilikuwaje uwaze jambo hili moyoni mwako? Petro alitumia swali hili kumkemea Anania. "Hukupaswa kuamua kuwa mwongo juu ya jambo hili." # Anania alidondoka chini na akakata roho Anania alianguka chini kwasababu alikufa. Hakufa kwasababu alianguka chini bali alikufa na kisha akaanguka chini.