# Ndipo wao wakarudi "Mitume wakarudi" # mwendo wa siku ya sabato Hii inaelezea umbali ambao kutokana na desturi za walimu wa sheria wa kiyahudi, mtu aliruhusiwa kutembea mwendo wa sabato ambao yapata kilomita moja hivi. # Walipowasiri "Walipofika mwisho wa safari yao. Mstari wa 12 unasema, "Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni" # chumba cha juu "chumba ambacho kipo juu kwenye nyumba" # Walikuwa wameungana kama mtu mmoja Kikundi kiliungana na hakikuwa na mgawanyiko au migongano. # wakiwa na juhudi wakiendelea katika kuomba Wanafunzi waliomba kwa pamoja kwa kawaida na mara kwa mara.