# Sentesi unganishi: Yesu aliendelea kuongea na umati kuhusu Yohana Mbatizaji. # Maelezo kwa ujumla Katika mstari wa 10, Yesu anamnukuru nabii Malaki kuonyesha kuwa maisha na huduma ya Yohana imetimiza unabii. # Lakini mliondoka kuona nini--nabii? Yesu anatumia swali ili kuwafikirisha watu juu ya Yohana mbatizaji kuwa ni mtu wa aina gani. "Lakinini kweli kwamba mlienda jajngwani kumuona nabii" # Lakini mlienda nje kuona nini--nabii? Ndiyo, nawaambia nyinyi. Kiwakilishi cha wingi ''nyinyi'' inarejelea kwa katika hali zote. # ni zaidi ya nabii Hii inaweza kutafsirika kama sentensi timilifu. "Siyo nabii wa kawaida" au ''siyo mtu wa kawaida'' au ''ni wa muhimu kuliko nabii wa kawaida'' # huyu ndiye aliye andikiwa Hii inaweza kutafsirika katik mfumo tendaji. "Hiki ndicho nabii Malaki aliandika zamamni za kale kuhusu Yohana mbatizaji" # namtuma mjumbe wangu Kiwakilishi ''na'' na ''wangu'' kinamrejea Mungu. Malaki ananukuu ambacho Mungu alisema. # mbele ya uso wako Kiwakilishi "wako" ni cha umoja kwa sababu Mungu alikuwa anasema juu ya Masihi katika nukuu.vPia "uso" inamaanisha nafsi timilifu, "mbele yako" au "kutangulia" # ataandaa njia yako Hii ni sitiari inayomaanisha kuwa mjumbe atawaandaa watu kupokea ujumbe wa Masihi.