# Maelezo ya Jumla: Yahwe anaendelea kumpatia Ezekieli ujumbe kwa nchi ya Israeli. # katilia mbali Hii inamaanisha kuua "ua" # mwenye haki ... mwovu Hii inarejea kwa watu wenye haki na waovu. "wale ambao ni wenye haki ... wale walio waovu" au "watu wenye haki ... watu waovu" # kutoka kwako "miongoni mwako" # upanga wangu utatoka kutoka kwenye ala yake dhidi ya Hii inamzungumzia Yahwe akifanya hawa watu kufa kana kwamba amewau hasa kwa upanga wake mwenyewe. # wenye miili wote Hapa "mwili" ni mfani kwa "watu" "watu wote" # kutoka kusini kwenda kaskazini Hii inarejea kwa eneo la kaskazini, na kusini, na maeneo yote ya katikati. "katika kila uelekeo" "kila mahali" # kwamba mimi, Yahwe, nimeutoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake Hii inamwongelea Yahwe akisababisha watu kufa kana kwamba amewaua kweli kwa upanga wake. # Hautarudi tena Hii inamzungumzia Yahwe haurudishi upanga wake kutoka kuwashambulia watu kana kwamba upanga ulikuwa mtu ambaye hakuwa ameshikilia upanga wenyewe kuurudisha kutoka kushambulia.