# Sentensi unganishi: Paulo anawakumbusha waumini wa Galatia kwamba Mungu aliwapa Roho wa Mungu wakati walipoamini injili kwa imani, siyo kwa matendo yao ya kushika sheria # Maelezo ya jumla Paulo anawakemea Wagalatia kwa kuwauliza swali la uchokozi na Kejeli # Nani amewawekea uchawi? Paulo anatumia swali la uchokozi kwa kusema kuw Wagalatia wanatenda kama kuna ameweka laana au uchawi. Haamini kwa hakika kwamba mtu mmoja ameweka uchawi kwao. "Mnaenenda kana kwamba mtu amewawekea uchawi" # Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu Huu ni mwendelezo wa hoja kutoka mstari 1. Paulo anajua majibu ya maswali anayoyauliza. # Mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa imani ambayo mliisikia? "Mlimpokea Roho, si kwa matendo kama sheria isemavyo, lakini kwa kuamini kile mlichosikia." # Je ninyi ni wajinga? Swali hili lenye jibu linaonesha mshangao wa Paulo na hata hasira yake kwa Wagalatia Wagalatia ni wajinga. "Ninyi (wingi) mu wajinga kweli!" . # katika mwili Neno mwili ni lugha ya picha linalomaanisha juhudi. "kwa juhudi zako" au "kwa kazi yako mwenyewe."