# Sentensi unganishi Mtume Paulo, mwandishi wa barua hii kwa makanisa yaliyoko katika maeneo ya Galatia. # Maelezo ya jumla Maneno 'ninyi,' 'nanyi' au 'yenu' hurejelea watu wa Galatia katika wingi wao. # Aliyemfufua yeye "Aliyemfufua Yesu Kristo" # Kufufuliwa Hapa inamaanisha ni kitendo cha kumfanya mtu aliyekuwa amekufa kuwa hai tena. # Ndugu Hapa inamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.