# kauli unganishi Kwasababu ya kile Paulo amekuwa akiwaandikia Waefeso, anawatia moyo namna gani kuishi maisha yao kama waamini na tena anasisitiza umoja wa waamini. # Kama mfungwa kwa ajili ya Bwana "kama mtu ambaye yuko gerezani kwa sababu ya uchaguzi wake wa kumtumikia Bwana" # Nawasihi ninyi kuishi maisha yanayoendana na wito Neno "ninyi" linamaanisha Waefeso waamini. AT: "Nawatia moyo ninyi kujitunza wenyewe kwa namna nzuri ya wito." # Kwa unyenyekevu mkubwa na upole na uvumilivu, mkichukuliana kila mmoja katika upendo "jifunzeni kuwa wanyenyekevu, wapole, waumilivu na kuchukuliana kila mmoja katika upendo" # Tunzeni umoja wa Roho katika kifungo cha amani "tafuteni kuishi pamoja kwa amani kuuhifadhi umoja wa Roho"