# Waefeso 02 Maelezo ya Jumla ## Muundo na upangiliaji Sura hii inazingatia maisha ya Mkristo kabla ya kumwamini Yesu. Kwa hiyo Paulo anatumia habari hii kuelezea namna maisha ya zamani ya mtu ilivyo tofauti na utambulisho mpya wa Mkristo "katika Kristo." (See: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/faith]]) ## Dhana maalum katika sura hii ### Mwili mmoja Paulo anafundisha kuhusu kanisa katika sura hii. Kanisa lina makundi mawili tofauti ya watu (Wayahudi na Wayunani). Wao sasa ni kundi au "mwili" mmoja. Kanisa linajulikana pia kama mwili wa Kristo. Wayahudi na Wayunani wameunganishwa katika Kristo. ## Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii ### Wamekufa katika makosa na dhambi" Paulo anafundisha kwamba wale ambao si Wakristo "wamekufa" katika dhambi zao. Dhambi huwafunga au huwafanya kuwa watumwa. Hii inawafanya kuwa "wamekufa" kiroho . Paulo anaandika kwamba Mungu huwafanya Wakristo kuwa hai katika Kristo. (See: [[rc://*/tw/dict/bible/other/death]], [[rc://*/tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc://*/tw/dict/bible/kt/faith]] and [[rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor]]) ### Maelezo ya kuishi kidunia Paulo anatumia njia nyingi za kuelezea jinsi ilivyo dunia ya wasio Wakristo. "Waliishi kulingana na njia za ulimwengu huu" na "wanaishi kulingana na kiongozi wa mamlaka ya hewa," "kutimiza matamanio mabaya ya asili yetu ya dhambi," na "kutekeleza matamanio ya mwili na ya akili. " ## Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii ### "(hilo) Ni zawadi ya Mungu" Wasomi fulani wanaamini "hilo" hapa linamaanisha kuokolewa. Wasomi wengine wanaamini kwamba ni imani ambayo ni zawadi ya Mungu. Kwa sababu ya maandishi ya Kigiriki, "hilo" inamaanisha kuokolewa na neema ya Mungu kupitia imani. ### Mwili Hii ni suala ngumu. "Mwili" ina uwezekano wa kuwa mfano wa asili ya dhambi ya mtu. Maneno ya "Wayunani kimwili" yanaonyesha Waefeso wakati mmoja waliishi bila ya kumjali Mungu. "Mwili" pia hutumiwa katika aya hii kutaja sehemu ya kimwili ya mwanadamu. (See: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/fles]]) ## Links: * __[Ephesians 02:01 Notes](./01.md)__ __[<<](../01/intro.md) | [>>](../03/intro.md)__