# Sentensi Unganishi: Paulo anawakumbusha waamini walivyokuwa hapa mwanzo na sasa namna walivyo mbele za Mungu. # Na ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wana dhambi kiasi cha kushindwa kumtii Mungu kwa namna ile ile wafu wasivyoweza kujishughulisha kimwili tena. # makosa na dhambi zenu Maneno "makosa" na "dhambi" kimsingi yanamaanisha kitu kile kile. Paulo anayatumia yote pamoja kuweka mkazo wa ukubwa wa dhambi ya watu. # hapo mwanzo mlienenda Hii inaelezea tabia ya namna watu walivyoishi # kwa kumfuata mtawala wa mamlaka ya anga Mtume Paulo anatumia neno "anga" kumaanisha tabia za ubinafsi na ufisadi wa watu waaishio humu duniani. # mtawala wa mamlaka ya anga Hii inamaanisha ibilisi au shetani # roho yake yule Sentensi "roho yake yule" inamaanisha ibilisi au shetani. # Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu, tulikuwa tukifanya mapenzi mwili na ya akili. Maneno "mwili" na "nia" yanawakilisha mwili wote. # wana wa ghadhabu Watu ambao Mungu amewakasirikia