# Sentensi unganishi Paulo anasimama mbele ya wakuu wa makuhani na wajumbe wa baraza. # Ndugu zangu Hii ina maana " Wayahudi." # Nimeishi mbele za Mungu na dhamiri njema mpaka leo "Mimi najua kuwa hata leo nimefanya kila kitu Mungu alichotaka mimi kufanya" # Anania Ni mtu tofauti na Anania anayetajwa sura ya 5:3 # ukuta uliopakwa chokaa Inamaanisha ukuta uliopakwa chokaa ili uonekane kuwa safi. Paulo anamwambia Anania kuwa anaonekana safi kama ukuta uliopakwa chokaa lakini ndani kumejaa uovu. # Umeketi kuhukumu ... kinyume cha sheria? Paulo anatumia swali ili kumdhihirisha Anania kuwa ni mnafiki.