# Maelezo ya jumla Mistari hii imetaja viwakilishi vingi vya majina kuelezea watu mbalimbali walio tajwa na mwandishi Luka. # katika kisiwa chote Walitembelea kisiwa chote kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wakiunena ujumbe wa Injili katika kila mji walimopita. # Pafo Ni mji Mkuu wa kisiwa cha Kapro mahali Liwali alikuwa akiishi. # Walimkuta Neno "Kumkuta" linamaanisha kuwa walimfikia bila ya kumtafuta. # Mtu fulani mchawi "Mtu aliyekuwa akifanya kazu ya uchawi" au "Mtu aliyekuwa akifanya mambo yasiyo ya kawaida katika fani ya kimazingaombwe" # ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu "Bar - Yesu" maana yake "Mwana wa Yesu". Hakukuwa na mahusiano yoyote ya karibu na Yesu Kristo". Jina Yesu lilikuwa ni jina la kawaida katkia wakati ule. # Mchawi huyu alishirikiana "Alikuwa mara kwa mara pamoja na" au "Alikuwa mara kwa mara akiambatana na" # Liwali Huyu alikuwa Kiongozi mtendaji Katika utawala mkoa wa dola ya Rumi. # aliyekuwa mtu mwenye akili Hii ni historia ya maisha ya Liwali Sergio Paulus. # Lakini Elima "yule mchawi" Huyu alikuwa Bar- Yesu, ambaly aliyekuwa akiitwa mchawi. # hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa "Hivyo ndivyo jina lake katika lugha ya kigriki" # aliwapinga; alijaribu kumgeuza "Aliwazuia akijaribu kumgeuza" # alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani "Alijaribu kumshawishi Liwali kuiacha imani ya ujumbe wa Injli"