# Sentensi unganishi Petro anaingia Yerusalemu na anaanza kuongea na Wayahudi wa huko. # Maelezo ya jumla Huu ni mwanzo wa tukio jipya katika simlizi # Sasa Linaashiria sehemu mpya ya simlizi # Ndugu "Ndugu" Linamaanisha waumini katika Yudea. # waliokuwa Yudea "Waliokuwa wakiishi mkoa wa Yudea" # Walikuwa wamelipokea neno la Mungu Linamaanisha kuwa Wamataifa walikuwa wameupokea ujumbe wa Injili kuhusu Yesu. "Waliamini ujumbe wa Mungu kuhusu Yesu Kristo". # Walikuwa wamepanda kwenda Yerusalemu Yerusalemu ilikuwa juu zaidi ya kila eneo la Israeli. hivyo ilikuwa kawaida kwa Waisraeli kusema wanapanda juu kwenda Yerusalemu. # lile kundi la watu waliotahiriwa Wayahudi walioamini kwamba kila anayeamini lazina atahiriwe. # watu wasiotahiriwa Linamaanisha, "watu wa Mataifa" # Alikula pamoja nao Ilikuwa kinyume kwa utamaduni wa Wayahudi, Wauahudi kula na Wamataifa.