# Kwa nje Hii inamaanisha mambo ya nje ya Kiyahudi ambayo watu wanayaona. # Siyo ya nje tuu katika mwili Hii inamaanisha mabadiliko ya nje katika mwili wa binadamu. # Ni Myahudi kwa ndani, na tohara ni ile ya moyoni Mistari hii miwili ina maana inayofanana. Mstari unaosema, "Ni Myahudi kwa ndani," inaelezea kuwa, "tohara ni ile ya moyoni." # Ndani Hii inaonyesha thamani na motisha ya mtu ambaye Mungu amembadilisha. # Kwa Roho, sio kwenye barua "Barua" ni sehemu ndogo ya maandishi katika lugha. Hapa inamaanisha maandiko. "kupitia kazi ya roho mtakatifu, sio kwa sababu unajua maandiko." # Kwa Roho Hii inaweza kuwa na maana ya ndani, sehemu yakiroho ya mtu, tofauti na nje "barua" ya sheria. Pia inamaana ya Roho Mtakatifu.