# Lakini wewe, Mungu, haujatukataa? Mwandishi anatumia swali hili kueleza huzuni yake kuwa inaonekana kwamba Mungu amewakataa. "Lakini Mungu, inaonekana kama umetukataa." au "Mungu, inaonekana kama umetuacha" # Hauendi vitani na jeshi letu Mwandishi anazungumzia Mungu kusaidia jeshi lao kana kwamba Mungu huwa anapigina pamoja nao. "huwa husaidii jeshi letu tunapoenda vitani" # haufai "hauna maana" # tutashinda "kuwa na ushindi" # atawakanyaga chini adui zetu Mwandishi anazungumzia Mungu kusaidia jeshi lao kuwashinda adui zao kana kwamba Mungu alikuwa akiwakanyaga adui zao. "atatusaidia kuwakanyaga chini adui zetu" au "atatuwezesha kuwashinda adui zetu"