# Wanarudi jioni Wanaorudi ni watenda maovu. # wanalia kama mbwa Mwandishi anazungumzia vitishio vya adui zake kushambulia watu kana kwamba walikuwa ni mbwa wanaolia, kunguruma, au kubweka kwa watu. "wanatishia kushambulia watu" # kuuzunguka mji "kuuzunguka mji kumshambulia yeyote watakayemkuta" # Tazama Hapa neno "Tazama" linatumika kuvuta nadhari kwa kitu. "Sikia" # wanateuka kwa midomo yao Kusema vitu viovu inazungumziwa kama kuteuka. Vitu hivi vibaya vinaweza kuwa ni matusi au vitisho. "wanasema vitu vibaya" au "wanapiga kelele kwa kusema vitu vibaya" # teuka kutoa pumzi kwa nguvu kutoka mdomoni; kuruhusu hewa kutoka tumboni kupitia mdomoni kwa sauti kubwa ya kuudhi. # panga ziko kwenye midomo yao Vitu vya ukatili ambavyo watu waovu walikuwa wakisema vinazungumziwa kana kwamba ni panga. "wanasema vitu vya ukatili vinavyosababisha watu taabu kama panga zinavyoangamiza watu" # Nani anatusikia? Swali hili linatumika kuonesha kuwa waliamini kuwa Mungu hatawasikia na kuwaadhibu. "Hakuna mtu anayetusikia!" au "Mungu wenu hatusikii!"