# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # weka katika Al Tashhethi Hii inaweza kuwa inaeleza mtindo wa muziki au tuni ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Michtamu Maana ya neno "michtamu" haiko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi ambayo Daudi aliandika" # Sauli alipotuma, na wakaangalia nyumba kumuua "katika kipindi Sauli alipowatuma askari wake kwenda na kuangalia nyumba ya Daudi kwa ajili ya nafasi ya kumuua" # niweke juu Sehemu ya juu inawakilisha sehemu salama ambapo adui zake hawawezi kumfikia. "niweke sehemu salama" # inuka dhidi yangu Kuinuka dhidi ya mtu inawakilisha kumshambulia. "wananishambulia" # watu wenye kiu ya damu ""watu wenye hamu ya kuua" au "watu wanaopenda kuua watu"