# Waovu wanapotoka hata walipokuwa tumboni ... wanaenda pembeni tangu kuzaliwa Hili ni wazo moja linaloelezwa kwa njia mbili tofauti. # wanapotoka Kufanya vitu vibaya inazungumziwa kana kwamba watu wanatembea kwenye barabara, na wanageuka na kukosea njia. "wanafanya makosa" # Sumu yao ni kama sumu ya nyoka Vitu viovu ambavyo watu wanasema vinazungumziwa kana kwamba ni sumu. "Maneno yao maovu yanasababisha shida kama sumu ya nyoka inavyowadhuru watu" # ni kama fira kiziwi anayezuia maskio yake watu waovu wasiosikia ushauri au kukemewa wanazungumziwa kana kwamba ni nyoka ambazo haziitikii muziki wa mganga. "wanakataa kusikiliza kama fira kiziwi inayozuia maskio yake" # fira kiziwi anayezuia maskio yake Fira asiyeitikia muziki wa mganga anazungumziwa kana kwamba inaweza kuweka kitu katika maskio yake ili kwamba isisikie. "fira asiye sikia" # fira aina ya nyoka mwenye sumu # waganga watu wanaocheza au kuimba muziki ili kumwongoza nyoka # haijalishi ujuzi wao ulivyo "haijalishi ujuzi walionao waganga katika kumwongoza nyoka"