# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # weka katika Al Tashhethi Hii inawezakuwa inaeleza mtindo wa muziki au tuni ya kutumia wakati wa kuimba zaburi hii. "imba zaburi hii kwa kutumia tuni ya 'Al Tashhethi'" au # Al Tashhethi Hii inamaanisha "Usiangamize." # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Michtamu Maana ya neno "michtamu" haiko wazi. Hii inaweza kuandikwa kama: "Hii ni zaburi aliyoandika Daudi." # alipotoroka kutoka kwa Sauli, katika pango "Hii ina husu Daudi alipojificha kwenye pango akimkimbia Sauli" au "Hii ina husu wakati mfalme Sauli alipokuwa anamfukuza Daudi, na Daudi akajificha kwenye pango" # ninakukimbilia Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi inazungumziwa kama kumkimbilia. "ninaenda kwako kwa ajili ya ulinzi" # ninakaa chini ya mbawa zako kwa ajili ya ulinzi Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba ni ndege anayelinda makinda yake kwa kuwaficha chini ya mbawa zake. "nakuamini wewe kunilinda" # hadi uharibifu wake uishe Mwandishi wa zaburi anazungumzia hamu ya Sauli kumuua kana kwamba Sauli alikuwa akitafuta kumwangamiza adui. "hadi shida hii iishe" au "hadi nitakapo kuwa siko hatarini tena"