# anaye nishikilia Kumtetea Daudi na kumweka salama inazungumziwa kama kumshikilia. "anaye nitetea" au "anaye niweka salama" # Atawalipa adui zangu kwa uovu Adhabu inazungumziwa kana kwamba ilikuwa ni malipo. "Atafanya uovu kwa adui zangu ambao walioufanya kwangu" au "Atasababisha uovu ambao adui zangu walifanya kwangu ufanywe kwao" # katika uaminifu wako, waangamize Hapa Daudi anabadilisha kutoka kuzungumza kumhusu Mungu na kuongea naye. "Mungu, waangamize kwa sababu wewe ni mwaminifu kwangu"