# O, kwamba wokovu wa Israeli uje Neno "O" hapa linatambulisha mshangao unaoonesha matumaini au ombi. "Natumaini kuwa wokovu wa Israeli utakuja" au "Ninaomba kwamba wokovu uje" # wokovu wa Israeli uje kutoka Sayuni Wokovu unaashiria Mungu, mwokozi, ambaye hekalu lake liko Sayuni. "mwokozi wa Israeli utakuja kutoka Sayuni" au "Mungu atakuja kutoka Sayuni na kuokoa Israeli" # Mungu atakapo warudisha watu wake kutoka mateka "Mungu atakapo okoa watu wake wafungwa" # Yakobo atasherehekea na Israeli kufurahi! Misemo hii miwili ina maana moja. # Yakobo Hapa "Yakobo" inamaanisha uzao wa Yakobo, Waisraeli.