# Sadaka za Mungu "Sadaka zinazompendeza Mungu" # roho iliyovunjika Roho iliyovunjika inawakilisha mtazamo wa unyenyekevu. "unyenyekevu" au "mtu anayekuwa mnyenyekevu" # moyo ulio vunjika na wenye majuto Kuwa mnyenyekevu na majuto juu ya dhambi za mtu inazungumziwa kama kuwa na moyo ulio vunjika na wa majuto. Moyo unawakilisha hisia na nia. "huzuni na unyenyekevu" au "mtu anayejuta kwa ajili ya dhambi zake na ni mnyenyekevu" # uzijenge kuta za Yerusalemu Kuta za mji huulinda mji na watu waliomo. Maana zinazowezekana ni 1) "utuwezeshe kujenga kuta za Yerusalemu" au 2) "ilinde Yerusalemu na uifanye kuwa imara" # watu wetu watatoa mafahali katika madhabahu yako Fahali ni ng'ombe dume. Mafahali mara nyingi hutumika kama wanyama wa sadaka, kulingana na maagizo ya Mungu.