# Tazama, nilizaliwa katika udhalimu ... tazama, unatamani uaminifu Matumizi mawili ya "Tazama" hapa yanavuta nadhari kati ya tofauti ya mambo haya mawili. "Hakika nilizaliwa katika udhalimu ... Lakini unatamani uaminifu" # Tazama, nilizaliwa katika udhalimu ... mara tu mama yangu alipochukua mimba yangu, nilikuwa katika dhambi Misemo hii miwili inamaana moja na inatumika pamoja kuleta msisitizo. # nilizaliwa katika udhalimu Kuwa mwenye dhambi inazungumziwa kama kuwa kwenye udhalimu. "nilikuwa mwenye dhambi tayari wakati nazaliwa" # mara tu mama yangu alipochukua mimba yangu, nilikuwa katika dhambi Kuwa mwenye dhambi inazungumziwa kama kuwa kwenye dhambi. "hata mama yangu alipobeba mimba yangu, nilikuwa mwenye dhambi" # unatamani uaminifu moyoni mwangu Moyo unawakilisha kati ya 1) hamu za mtu au 2) mtu mzima. "Unataka nitamani uaminifu" au "unataka niwe mwaminifu"