# Fariji, fariji Neno "fariji" linarudwa kwa ajili ya msisitizo # asema Mungu wako Hapa "wako" ni wingi na ina maana ya wale ambao nabii anawaambia kufariji watu wa Mungu. # Zungumza kwa upole kwa Yerusalemu Nabii anazungumzia Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mwanamke ambaye Yahwe alimsamehe. Kwa hiyo, Yerusalemu inawakilisha watu wanaoishi katika mji huo. Zungumza kwa upole kwa watu wa Yerusalemu" # tamka kwake ...ustawi wake ... udhalimu wake amepokea ... dhambi zake Viwakilishi nomino vina maana ya Yerusalemu lakini inaweza kubadilishwa kama "watu wa Yerusalemu" inaazimwa kama tafsiri. "tangaza kwao ... ustawi wao ... udhalimu wao ... wamepokea ... dhambi zao" # ustawi wake Maana zaweza kuwa ya kwamba neno "ustawi" lina maana ya 1) kwa vita ya kijeshi au 2) kwa kazi ya kulazimishwa. # udhalimu wake umesamehewa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe amesamehe udhalimu wake" # kutoka mkononi mwa Yahwe Hapa neno "mkono" inawakilisha Yahwe mwenyewe. "kutoka kwa Yahwe"