# Bwana Yahwe, Yahwe Mungu Katika Agano la Kale, "Bwana Yahwe" mara kwa mara limetuika limerejea kwa Mungu wa kweli mmoja." # nyumba Neno "nyumba" mara nyingi limetumika katika Biblia. * Wakati mwingine linamaanisha "kaya," kurejea watu waishio pamoja katika nyumba moja. * Mara nyingi "nyumba" hurejea kwa ukoo wa mtu au ndugu wengine. Kwa mfano, kirai "nyumba ya Daudi" hurejea kwa koo zote za Mfalme Daudi. * Maneno "nyumba ya Mungu" na "nyumba ya Yahwe" hurejea kwa hema au hekalu. Haya maelezo pia unaweza kurejea kiujumla mahali Mungu alipo au makao. # Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli Neno "Israeli" ni jina ambalo Mungu alipatia Yakobo. Lina maana, "amepigana na Mungu."