# Warumi 05 Maelezo ya Jumla ### Muundo na upangiliaji Wasomi wengi wanaona mistari ya 12-17 kama baadhi ya vifungu muhimu zaidi, lakini vigumu kuelewa, katika Maandiko. Baadhi ya ukwasi na maana yao labda imepotea wakati wa kutafsiriwa kutoka kwa jinsi Kigiriki cha awali kilikuwa. ### Dhana maalum katika sura hii #### Matokeo ya kuhesabiwa haki Jinsi Paulo anavyoeleza matokeo ya kuhesabiwa haki ni sehemu muhimu ya sura hii. Matokeo haya ni pamoja na kuwa na amani na Mungu, kuwa na uwezo wa kumfikia Mungu, kuwa na uhakika juu ya kesho, kuwa na furaha wakati wa kuteseka, kuokolewa milele, na upatanisho na Mungu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/justice) #### "Wote wametenda dhambi" Wasomi wamegawanyika juu ya kile Paulo alimaanisha katika mstari wa 12: "Na kifo kilienea kwa watu wote, kwa sababu wote walitenda dhambi." Wengine wanaamini kuwa watu wote walikuwapo katika "uzao ya Adamu." Kwa hiyo, kama Adamu ni baba wa wanadamu wote, watu wote walikuwapo wakati Adamu alifanya dhambi. Wengine wanaamini kwamba Adamu alikuwa mwakilishi wa wanadamu. Kwa hiyo, alipotenda dhambi, watu wote "walianguka" kwa sababu hiyo. Ikiwa watu leo ​​walihusika au kutohusika katika dhambi ya awali ya Adamu, ni tofauti moja kati ya maoni haya. Vifungu vingine vitasaidia mtu kuamua. (See: rc://en/tw/dict/bible/other/seed]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc://en/ta/man/translate/figs-activepassive) #### Adamu wa pili Adamu alikuwa mtu wa kwanza na "mwana" wa kwanza wa Mungu. Aliumbwa na Mungu. Alileta dhambi na kifo ulimwenguni kwa kula matunda yaliyokatazwa. Paulo anaelezea Yesu kama "Adamu wa pili" katika sura hii na mwana wa kweli wa Mungu. Yeye huleta uzima na alishinda dhambi na kifo kwa kufa kwenye msalaba. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/sonofgod]] and [[rc://en/tw/dict/bible/other/death) ## Links: * __[Romans 05:01 Notes](./01.md)__ __[<<](../04/intro.md) | [>>](../06/intro.md)__