# Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema Neno "sauti" inamaanisha yule anayezungumza. "mtu akinena kwa sauti kutoka katika kiti cha enzi akisema" # Tazama! Nenno "Tazama" inatuweka macho kuwa makini na taarifa za kushangaza zifuatazo. # Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na inasisitiza kuwa, hakika, Mungu ataishi miongoni mwa watu. # Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao Machozi hapa yanawakilisha huzuni. "Mungu atafuta huzuni yao kama vile anafuta machozi yao" au "Mungu atawasababisha wasiwe na huzuni tena"