# Taarifa ya Jumla: Katika mistari hii, neno "wa" inamaanisha mabaharia na wanamaji, na yule mtu mmoja anayezungumziwa ni ule mji wa Babeli. # Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa? Swali hili linawaonesha watu umuhimu wa mji wa Babeli. "Hakuna mji mwingine kama mji ule mkuu, Babeli" # Mungu ameleta hukumu yenu juu yake Nomino "hukumu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuhukumu." "Mungu amemuhukumu kwa ajili yenu" au "Mungu amemuhukumu kwa sababu ya maovu aliyowatendea"