# shimo lisilo na mwisho Hili ni shimo refu sana. Maana zinazowezekana ni 1)shimo halina mwisho chini; inaendelea kwenda chini zaidi milele au 2) shimo ni refu sana hata linakuwa kana kwamba halina mwisho. # Kisha ataendelea na uharibifu Nomino "uharibifu" inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "Kisha ataangamizwa" au "Kisha Mungu atamuangamiza" # ataendelea na uharibifu Uhakika wa kile kitakachotokea baadae kinazungumziwa kana kwamba mnyama anaendako. # wale ambao majina yao hayakuandikwa "wale ambao majina yao hayajaandikwa na Mungu" # tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu "kabla Mungu hajaumba ulimwengu"