# mbinguni au duniani au chini ya dunia Hii inamaanisha mahali pote: Mahali ambapo Mungu na malaika huishi, mahali ambapo watu na wanyama huishi, na mahali ambapo wale waliokufa walipo. # Tazama "Sikiliza" au "kuwa makini na jambo nilotaka kukuambia" # Simba wa kabila ya Yuda Hili ni jina la mtu kutoka kabila la Yuda ambaye Mungu aliahidi atakuwa mfalme mkuu. "Yule aitwaye Simba wa kabila la Yuda" au "Mfalme aitwaye Simba wa kabila la Yuda" # Simba Mfalme anazungumziwa kama vile yeye ni simba kwa sababu simba ni mnyama imara sana. # shina la Daudi Huyu ni mzawa wa kizazi cha Daudi ambaye Mungu aliahidi atakuwa mfalme mkuu. "yule aitwaye shina la Daudi" # shina la Daudi Huyu mzawa anazungumziwa kama vile familia ya Daudi ni mti na yeye ni shina lake.