# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Sikia ombi langu Maneno "ombi langu" ni njia nyingine ya kusema mtu anaye omba. "Nisikilie ninapoomba kwako" au "Kuwa tayari kufanya ninachokuomba kufanya" # nijibu "tafadhali fanya ninachokuomba ufanye" # Usiingie hukumuni "Tafadhali usinihukumu" au "Nakusihi usinihukumu" # mtumishi wako Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba anamzungumzia mtu mwingine. "mimi" # machoni pako hakuna aliye na haki "haufikiri kuwa yeyote ana haki"