# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Moyo wangu uko thabiti, Mungu Hapa Daudi anajitambulisha kwa moyo wake. Pia, neno "thabiti" inamaanisha kuamini kabisa. "Moyo wangu uko thabiti kwako, Mungu" au "Nakuamini wewe kabisa, Mungu" # Nitaimba sifa pia na moyo wangu uliotukuzwa Hapa Daudi anajitambulisha kama kuwa na heshima ya kumsifu Mungu. "Unaniheshimu kwa kuniruhusu kukuimbia sifa" # Amka, kinanda na kinubi Hapa Daudi anaeleza kucheza vyombo kama kutembea kutoka usingizini. "Nitakusifu kwa kucheza kinanda na kinubi" # Nitaamsha alfajiri Hapa Daudi anaeleza alfajiri kuamka kama mtu kuamka asubuhi. "Nitakuwa nikikusifu alfajiri ifikapo" # alfajiri jua linapochomoza.