# Mbingu zinasifu Hapa "mbingu" inawakilisha wale walio mbinguni. # zinasifu maajabu yako, Yahwe "zinakusifu, Yahwe, kwa sababu ya mambo ya ajabu unayotenda" # ukweli wako unasifiwa katika kusanyiko la watakatifu wako "Mkusanyiko wa watakatifu hukusifu kwa sababu daima huwa unafanya ulichoahidi kufanya" # kusanyiko la watakatifu wako Hii inamaanisha malaika mbinguni. # Kwa kuwa ni nani angani anaweza kulinganishwa na Yahwe? Nani miongoni mwa wana wa miungu ni kama Yahwe? Maswali haya yote yana maana moja. Mwandishi anatumia swali hili kusisitiza kuwa hakuna mtu kama Yahwe mbinguni. # wana wa miungu Hapa "wana" inamaanisha kuwa na sifa za. HIi ni njia ya kumaanisha viumbe vya kiroho vinavyoishi mbinguni. "malaika" au "viumbe vitakatifu"