# Taarifa ya Jumla: Hapa Mungu anaanza kuzungumza. # Nilitoa mzigo kutoka mabegani mwake Hapa "mzigo kutoka mabegani mwake" inawakilisha kazi za kulazimishwa ambazo Waisraeli iliwalazimu kufanya kama watumwa Misri. # mikono yake iliwekwa huru na kushikilia kikapu Hapa "kushikilia kikapu" inawakilisha kazi za kulazimishwa ambazo Waisraeli iliwalazimu kufanya kama watumwa Misri. # katika dhiki yako "katika mateso yako makuu" # Nilikujibu kutoka katika wingu la giza la radi Mungu alipokuja kwa Waisraeli, alificha ukamili wa uwepo wake na utukufu katika wingu lenye giza na la kutisha. # Nilikujaribu katika maji ya Meriba Mungu aliwajaribu wana wa Israeli kuona kama watamtumaini kuwapa maji katika jangwa la Meriba.