# Usishikilie dhambi za baba zetu dhidi yetu "Usiendelee kukumbuka dhambi za baba zetu na kutuadhibu kwa sababu yao" au "Tusamehe kwa dhambi za baba zetu" # tuko chini sana "tumedhoofika sana" # Mungu wa wokovu wetu "Mungu anayetuokoa" # kwa ajili ya utukufu wa jina lako Neno "jina" ni njia nyingine ya kusema sifa yake, kwa kile ambacho watu wanachojua kumhusu. "ili watu wajue kuhusu utukufu wako" # kwa ajili ya jina lako Jina la Mungu hapa linamwakilisha yeye na heshima anayostahili. "ili watu wakuheshimu" au "kwa ajili yako mwenyewe"