# tuma nuru yako na ukweli wako Mwandishi anazungumzia ukombozi wa Mungu kana kwamba ni nuru inayo mwonyesha njia na ukweli unaomfundisha jinsi ya kuishi. "niongoze kwa nuru yako na kweli" # mlima ... mtakatifu Hii inamaanisha mlima ulioko Yerusalemu ambapo hekalu lipo kwa hiyo ni hekalu lenyewe. # kwenye makazi yako "mahali ambapo unaishi" # Mungu furaha yangu inayozidi "Mungu ambaye ni furaha yangu kubwa sana" au "Mungu anayenipa furaha kubwa"