# Taarifa ya Jumla: Daudi anaendelea kueleza kile amabacho hatia na aibu yake inavyoufanya mwili wake. Anatumia kauli iliyokuzwa kuweka mkazo madhara ya somo hili. # hakuna afya katika mifupa yangu kwa sababu ya dhambi yangu Hapa "mifupa yangu" inawakilisha mwili wa mwandishi. "mwili wangu wote unaugonjwa kwa sababu ya dhambi yangu" # udhalimu wangu unanilemea Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni mafuriko ya maji yanayomfunika. "udhalimu wangu unanifunika kama mafuriko" # ni mzigo mzito sana kwangu Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni mzigo asioweza kuinua. "ni kama mzigo ulio mzito sana kwangu kunyanyua"