# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Yahwe ni nuru yangu Hapa "nuru" inawakilisha maisha. "Yahwe ni chanzo cha maisha yangu" # nimwogope nani? Swali hili linaweka mkazo kuwa hakuna mtu ambaye Daudi anapaswa kumwogopa. "sitamwogopa mtu yeyote" # Yahwe ni kimbilio langu Hii inamzungumzia Yahwe kana kwamba ni sehemu ambapo watu wanaweza kwenda kwa ajili ya usalama. "Yahwe ndiye anayeniweka salama" # nimhofu nani? Swali hili linaweka mkazo kuwa hakuna mtu ambaye Daudi anapaswa kumwogopa. "sitamhofua mtu yeyote"