# Taarifa ya Jumla: Zaburi hii inaendelea kueleza jinsi Mungu anavyotujali kama kondoo anavyowajali kondoo wake. # Hurudisha maisha yangu Hii inamaanisha Mungu anamfanya mtu aliyenyonge na mchovu kuwa na nguvu na kupumzika tena. # huniongoza katika njia zilizonyooka Kumwonyesha mtu jinsi ya kuishi katika njia inayo mpendeza Mungu inazungumziwa kana kwamba ni mchungaji anaonesha kondoo njia sahihi ya kuchukua. "Ananionesha jinsi ya kuishi sawa" # kwa ajili ya jina lake Msemo "jina lake" hapa unamaanisha sifa yake. "kwa ajili ya jina lake" au "ili watu wamheshimu"