# unamletea baraka nyingi Nomino dhahania "baraka" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "unambariki sana" au "unampa vitu vingi vizuri" # umeweka kichwani mwake taji la dhahabu safi Kuweka taji juu ya kichwa cha mtu ni ishara ya kumfanya kuwa mfalme. # taji la dhahabu safi Hapa "dhahabu safi" inaashiria heshima kubwa anayopewa mfalme. # Aliomba uhai; ukampa Nomino dhahania ya "uhai" inaweza kuelezwa kama kitenzi. "Alikuomba kuwa umfanye aishi kwa muda mrefu, ukaifanya itokee" # siku ndefu milele na milele Maana zinazowezekana ni 1) maisha marefu sana au 2) masiha ya milele au 3) uzao mrefu.