# Maelezo ya Jumla: Mika anaendelea kuongelea hukumu juu ya manabii wa uongo. # itakuwa usiku kwenu...siku itakuwa giza juu yao Yahwe anasema katika 3:6 hawa manabii wa uongo hawatapokea tena ujumbe wa Mungu kwa watu wa Israeli. Wakati mwingine manabii walipata ujumbe kutoka kwa Mungu kupitia maono, au ndoto usiku. # Waonaji watawekwa kuwa aibu, na waaguzi watachanganyikiwa "Nitawafanya waonaji kuwa aibu, na nitawachanganya waaguzi" # Wote watafunga midomo yao "Hawataongea tena" # kwa kuwa hakuna jibu kutoka kwangu Hii inamaanisha Mungu atakuwa kimya kama sehemu ya adhabu yao.