# Kwa maneno yako mwenyewe "Kutokana na ulichokisema" # Kwamba mimi ni mtu mbaya, nachukua Afisa alirudia maneno aliyoyasema mtumishi juu yake. Hakusema kuwa ilikuwa kweli. # Mtu mkali "mtu mkorofi" # Kwa nini hukuweka pesa yangu...... faida? Afisa alitumia swali ili kumkemea Mtumishi dhalimu. "Ungeweka pesa yangu..... faida." # Weka pesa yangu benki "Kopesha pesa zangu benki" Tamaduni ambazo hazina benki zaweka kutafsiri kuwa "Acha mtu aazime pesa zangu." # Benki Benki ni biashara salama ya kuweka pesa za watu. Benki huwakopesha watu pesa kwa faida. Hivyo inalipa pesa ya ziada au faida kwa watu wanaoweka pesa zao benki. # Nitakusanya na faida "Ningekusanya kiasi hicho cha fedha pamoja na faida iliyopatikana" au "ningepata faida" # Faida Faida ni pesa ambayo benki humlipa mtu anayeweka pesa zake katika benki.