# kukaa huko mwaka Yakobo anazungumzia kutumia mda kama pesa. "kaeni huko mwaka mzima" # Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho Yakobo anatumia swali hili kuisahihisha hadhira yake. "Hakuna ajuaye kitakachotokea kesho" # maisha yenu ni nini hasa? Yakobo alitumia swali hili kufundisha waamini kuwa maisha ya kimwili sio ya muhimu sana. "fikirini juu ya maisha yenu ya kimwili" # Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea. Yakobo anawafananisha watu na ukungu ambao hutokea na kupotea kwa haraka. "mnaishi kwa muda mfupi na kufa"