# Sentensi unganishi: Yakobo anaendelea kuwaambia waamini wa Kiyahudi waliotawanyika namna ya kuishi kwa kupendana na kuwakumbusha kutowapendelea matajiri juu ya masikini. # Ndugu zangu Yakobo anawaandikia ndugu zake ambao ni waamini wa Kiyahudi . "waamini wenzangu" au "ndugu zangu katika Kristo" # Ishikeni imani ya Bwana Yesu Kristo Mwamini Yesu Kristo. # Bwana wetu Yesu Kristo Neno "wetu" linamaanisha Yakobo na waamini wenzake. # upendeleo kwa watu wengine shauku ya kumsaidia mtu fulani zaidi ya mwingine # Kama mtu fulani Yakobo anaanza kuelezea hali ambayo waamini wanamthamini sana tajiri kuliko masikini. # amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri "amevaa kama mtu tajiri" # keti hapa mahali pazuri "keti hapa sehemu ya heshima" # simama pale "hamia sehemu isiyo na heshima" # Kaa chini ya miguu yangu Hamia sehemu ya kunyenyekea # Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya? Yakobo alitumia swali kuwakemea wasomaji wake. "Mnahukumiana wenyewe kwa wenyewe na kufanya maamuzi mkiwa na mawazo mabaya"