# Nisikilize mimi Hapa "mimi" ina maana ya Yahwe # ambao wamebebwa na mimi kabla ya kuzaliwa kwako, kubebwa kutoka tumboni Yahwe anazungumzia taifa la Israeli kana kwamba lilikuwa mtu, na mwanzo wa taifa kana kwamba ni kuzaliwa kwake. # ambao wamebebwa na mimi Yahwe anazungumzia kusaidi na kuokoa watu wa Israeli kana kwamba alikuwa akiwabeba. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ambao nimewabeba" # Hata katika uzee wako mimi ndiye, na mpaka nywele zako ni mvi nitakubeba Yahwe anazungumzia taifa la Israeli kuwa zee sana kana kwamba likikuwa mwanamume mzee mwenye mvi.