# hivyo katikati mwa maisha yangu "ya kuwa kabla sijawa mzee". Hii ina maana ya kufa katika umri wa kati, kabla ya kuzeeka. # Nitapita katikati ya malango ya kuzimu Hii inazungumzia kufa kana kwamba kuzimu ilikuwa ufalme ambao una malango ambayo mtu huingia. "Nitakufa na kuelekea kuzimu" # Nimetumwa kule kwa miaka yangu iliyobaki Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kabla sijaishi miaka yangu yote nitaenda kaburini" # katika nchi ya wanaoishi "Wanaoishi" ina maana ya watu ambao wapo hai" au "katika dunia hii ambamo watu wapo hai"