# Taarifa ya Jumla Kamanda mkuu anaendelea kuzungumza ujumbe wa mfalme wa Ashuru kwa watu wa Yuda. # Je! kuna miungu yoyote ya watu iliyowaokoa kutoka .... Ashuru? Kamanda mkuu anatumia swali hili kudhihaki watu wa Yuda. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "hakuna kati ya miungu ya watu iliyowaokoa wao kutoka .... Ashuru" # mkono wa mfalme Utawala wa mfalme una maana ya "mkono" wake. "utawala wa mfalme" # Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Wako wapi miungu wa Sefarvaimu? Je! wameokoa Samaria kutoka katika nguvu yangu? Kamanda mkuu anatumia maswali haya kudhihaki watu wa Yuda. Maswali haya yanaweza kuunganishwa na kuandikwa kama kauli. "Miungu ya hamathi, Arpadi, Sefravaimu, na Samaria haikuokoa watu wao kutoka katika nguvu yangu" # Hamathi ... Arpadi Haya ni majina ya miji. # Sefarvaimu Hili ni jina la mji. # Je! kuna mungu yeyote ambaye amekuokoa ... kana kwamba Yahwe anaweza kuokoa Yerusalemu kutoka katika nguvu yangu? Kamanda mkuu anatumia swali hili kudhihaki watu wa Yuda. Swali hili linaweza kuandikwa kama kauli. "Hakuna mungu ambaye amekuokoa ... na Yahwe hatakuokoa Yerusalemu kutoka katika nguvu yangu" # nchi yake Hii ina maana ya watu ambao wanaishi katika nchi. "watu wake"