# Taarifa ya jumla: Bwana anazungumza juu ya Israeli. # Efraimu alijiunga na sanamu; mwache peke yake Efraimu ni watu wa kaskazini mwa ufalme wa Israeli. Walichagua kuabudu miungu badala ya Bwana. Bwana anamuamuru Hosea asijaribu kuwarekebisha maana hawatasikia. # watawala wake hupenda sana aibu yao Viongozi hawaoni aibu ya kile walichokifanya wanapoabudu miungu na kugeuka dhidi ya Bwana. # Upepo utamfunga kwa mabawa yake Hapa "upepo" unawakilisha hukumu ya Mungu na hasira juu ya taifa la Israeli. Bwana ataruhusu maadui wawashinde watu wa Israeli na kuwachukua mateka.