# wenye mwili Maana yaweza kuwa 1) wanadamu wote au 2) viumbe vyote vyenye mwili, ikijumlisha wanadamu na wanyama. # inchi imejaa ghasia kutokana na wao "watu nchini kote wana vurugu" # nitawaangamiza wao pamoja na nchi "Nitawaangamiza wao pamoja na nchi" au "Nitawaangamiza wao nitakapoiangamiza nchi" # safina Hii inamaanisha sanduku kubwa sana ambalo lingeweza kuelea juu ya maji hata katika dhoruba mbaya. "mtumbwi mkubwa" au "meli" au "tishali" # mti wa mvinje Watu hawajui haswa huu ulikuwa mti wa aina gani. "mbao iliyotumika kuunda mitumbwi" au "mbao nzuri" # vifunike kwa lami "sambaza lami juu yake" au "paka lami juu yake". Sababu ya kufanya hivi yaweza kuwekwa wazi: "kufanya isipitishe maji" # lami Hiki ni kimiminiko chenye mafuta, kizito, na kinatacho ambacho watu huweka nje ya mtumbwi kuzuia maji kupenya katika nafasi za mbao hadi kwenye mtumbwi. # dhiraa Dhiraa ilikuwa ni namba ya kipimo, kiasi kidogo tu kwa mita moja. # dhiraa mia tatu "mita 138". Dhiraa mia tatu ni sawa na mita 138" # dhiraa hamsini "mita ishirini na tatu" # dhiraa thelathini "mita kumi na nne"