# Maelezo ya Jumla: Yahwe anaendelea kumpatia Ezekieli ujumbe wake kwa viongozi wa Israeli. # Kwa hiyo, wachungaji, lisikilizeni neno la Yahwe Tazama tafsiri yake katika sura ya 34:7. # Tazama! Neno "Tazama" hapa linaongeza msisitizo kwa kile kifutacho. # Niko juu ya wachungaji "nitawaadhibu wachungaji." # nitalitaka kundi langu kutoka mkononi mwao "nitawaadhibu kwa mambo yote mabaya waliyaacha kutokea kwa kundi langu." # nitawasitisha mbali na kuchunga kundi "sitawaacha kulichunga kundi tena" # watajichunga wenyewe "kujilisha na kujichunga wenyewe" # kutoka vinywani mwao "hivyo hawataweza kuwala." # kundi langu halitakuwa chakula chao tena "wachungaji hawatawala tena kondoo na mbuzi wa kundi langu"