# Maelezo ya Jumla: Fumbo la Yahwe kuhusu mwerezi linaendelea. # Kimo chake kikubwa kilikuwa zaidi kuliko miti mingine yote katika shamba "Mwerezi ulikuwa mrefu kuliko miti mingine yote ya shambani" # matawi yake yakawa mengi "ulimea matawi mengi sana" # kwa sababu ya maji mengi ilimea "kwa sababu ulikuwa na maji mengi" # Kila ndege wa mbinguni alitengeza kiota kwenye matawi yake "Iina zote za ndege warukao angani walitengeza viota katika matawi yake" # wakati kila kiumbe hai cha shambani kilizaa mtoto chini ya tawi "na viumbe vyote viishivyo katika shamba walizaa chini yamatawi ya mwerezi" # Mataifa mengi yote yaliishi chini ya kivuli chake "mataifa yote yenye nguvu yaliishi katikakivuli chake" # ulikuwa uzuri katika ukuu wake na kimo cha matawi yake "Ulikuwa mzuri kwa sababu ulikuwa mkubwa na matawi yake yalikuwa marefu sana"